Simba yaipigisha kwata Polisi Dodoma
Na Ikram Khamees, Dodoma
Magoli mawili yaliyofungwa na Abdi Banda na Said Ndemla kila kipindi, yametosha kabisa kuwapigisha kwata Polisi Dodoma iliyokubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Vijana wa Simba wanaonolewa na Mcameroon, Joseph Omog walicheza kandanda safi na la kuvutia na kufanikiwa kujipatia mabao hayo mawili.
Simba imeamua kuelekea Dodoma ikiwa katika harakati zake za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli ambaye ameamua kuihamishia serikali yake mjini Dodoma