Shabiki mwenye vituko wa DRC anyimwa viza

Shabiki wa soka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Michel Kuka Mboladinga, anayejulikana sana kama Lumumba Vea, amewaambia wafuasi wake kuwa hataweza kusafiri kwenda Mexico kuiunga mkono timu ya taifa, baada ya kunyimwa viza.

Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 53 alijitokeza hadharani kwa kushangilia kama sanamu wakati wa Mashindano ya mwisho ya AFCON nchini Morocco.

Katika ujumbe mzito kwenye mitandao ya kijamii, Mboladinga alielezea kwa kina juhudi kubwa za nchi nyingi kufikia mashindano hayo.

Lumumba Vea alifahamika kwa kufanana kwake na Patrice Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mtu mkuu katika vita vya kupigania uhuru wa nchi hiyo.

DR Congo itaingia dimbani leo kucheza mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu kombe la Dunia, mashindano yatakayofanyikia Marekani, Mexico na Canada.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons