Ruka hadi kwenye maudhui makuu

CAF yaanzisha mashindano mapya

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametangaza rasmi kuanzishwa kwa mashindano mapya ya kimataifa yatakayojulikana kama African Nations League, yenye lengo la kuongeza ushindani na mapato katika soka la Afrika.

Mashindano hayo mapya yanachukua nafasi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN), huku yakibuniwa kwa mfumo mpya utakaoleta ushindani mkubwa zaidi na kushirikisha wachezaji wa viwango vya juu wanaocheza ndani na nje ya bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Motsepe, mashindano hayo yatakuwa na mifumo miwili tofauti ambapo wa kwanza African Nations League Continental, utaendeshwa kwa mfumo wa kanda ambapo timu bora kutoka kila ukanda zitashindana na hatimaye kupata washindi watakaoingia hatua ya fainali itakayofanyika katika nchi mwenyeji.

Pili, African Nations League Pan-African, utakuwa na muundo unaofanana na AFCON, ukizikutanisha timu bora zaidi barani Afrika pamoja na wachezaji nyota wanaocheza katika ligi kubwa duniani.

Motsepe amesema lengo la mashindano hayo ni kuongeza ushindani, kukuza vipaji vya wachezaji wa Afrika, pamoja na kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi katika soka la bara hilo.

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa CAF inaendelea na mazungumzo na FIFA pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha ratiba ya soka duniani inaruhusu mashindano hayo kufanyika bila kuathiri ligi za ndani ambazo tayari zina msongamano wa mechi.

Mashindano hayo mapya yanatarajiwa kuleta sura mpya katika soka la Afrika na kuongeza hadhi ya mashindano ya kimataifa ya bara hilo.




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe