Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amesema Coco Beach haijauzwa, bali serikali inaboresha ili kulipa hadhi eneo hilo na kudhibiti shughuli zisizokubalika kisheria.
"Vijana wengi waliopo pale Coco Beach hawana kazi hawana biashara wanazurura tu na wengine ni walevi wengine wanatumia bangi na wengine wanajiuza sasa tunaishukuru jeshi la polisi kwa kufanya upembuzi yakinifu na kutusanua juu ya hili jambo hivyo sisi kama manispaa ya kinondoni tumeamua kuifanya hili eneo liwe la kistaarabu kwa kuleta wawekezaji wapya ili kuwe na usalama zaidi"
