Klabu ya Simba SC imeweka wazi mpango wake wa kukata rufaa dhidi ya mchezaji wa Yanga SC, Mohamed Damaro ikitaka ipewe alama tatu huku pia iliitaka TFF kuipoka Yanga alama zaidi kutokana na mchezaji huyo kushiriki katika mechi nyingine.
Simba SC wameorodhesha hatua 6 ambazo zinafuatwa katika mchakato wa kuhama Shirikisho kwa mchezaji kwa mujibu wa FIFA, ambazo hazikufuatwa.
Kwa mujibu wa Regulations Governing the Application of the Statutes (RGAS), maombi ya kubadilisha Shirikisho lazima yapelekwe kwa Players’ Status Committee (PSC)
Kuna aina 4, lakini nimechukua hii ambayo Damaro inamhusu tu.
b) Kwa wachezaji wanaotaka kubadili chama cha soka (association) baada ya tayari kushiriki katika mashindano rasmi, katika ngazi yoyote au aina yoyote ya mpira wa miguu, kwa niaba ya chama kingine (Kifungu cha 9 aya ya 2 ya RGAS)
Mohamedi Damaro Camara ana angukia kipengele (b), kwani akiwa Guinea alishacheza vilabu vya HAFIA FC na MILO FC, lakini mwaka 2019 alikuwemo kwenye kikosi cha Guinea cha U17.
1. Kutuma maombi (FA)
2. Kupitiwa na Katibu wa FIFA
3. Maamuzi ya Players’ Status Committee
4. Vigezo vya maamuzi ya PSC
5. Msingi wa maamuzi ya PSC
6. Rufani CAS.
Simba SC wanaenda mbali na kusema kwenye Kanuni, Hadhi na Uhamisho wa wachezaji- RSTP) kifungu cha 9 ukurasa wa 78 na 79 hakikufuatwa kwenye usajili wa Damaro, ambacho kinasem
“Mara tu taarifa zote husika zitakapowekwa na nyaraka za lazima kupakiwa, klabu husika zitapaswa kuthibitisha uhamisho huo katika TMS bila kuchelewa na kabla ya mwisho wa kipindi cha usajili cha chama kipya (kwa kuzingatia masharti ya kipekee yaliyobainishwa katika Kifungu cha 6 cha kanuni hizi)”
FOREIGNER PLAYERS
1. Djigui Diarra
2. Pacome Zouzoua
3. Max Mpia Nzengeli
4. Chadrack Boka
5. Duke Abuya
6. Frank Assinki
7. Prince Mpumelelo Dube
8. Lassine Kouma
9. Allan Okello
10. Laurindo Dilson Maria
11. Buba Jammeh
12. Yao Kouassi Attohoula
13. Mohamed Damaro Camara
Simba inataka Yanga SC ipokwe alama, wanasema Damaro hajasajiliwa KIHALALI ni Raia wa Guinea kısoka.




