Samson Adamu kukaimu ukatibu mkuu CAF

CAF: Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limemteua Samson Adamu raia wa Nigeria, kuwa Katibu Mkuu wa muda, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa awali, Veron Mosengo-Omba.

Veron Mosengo-Omba ametangaza rasmi kujiuzulu na kustaafu baada ya kudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano tangu mwaka 2021.

Uteuzi huo uliothibitishwa leo unaashiria kuongezeka kwa ushawishi wa taifa la Nigeria katika maamuzi ya juu ya soka la Afrika, huku Adamu akitarajiwa kuchukua majukumu muhimu ya kiutawala katika taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Adamu anakuwa Mnigeria wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa CAF zaidi ya miaka 70 iliyopita.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI