Mkude aishitaki Yanga, TFF


Kiungo mkabaji wa zamani wa timu za Simba, Yanga na Taifa Stars, Jonas Gerard Mkude bado hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na sakata lake la madai dhidi ya timu yake ya zamani ya Yanga SC.

Inaelezwa kuwa Mkude amefungua kesi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akidai alipwe fedha anazodai kabla hajafanya maamuzi ya kujiunga na klabu nyingine yoyote.

Kutokana na hilo, Mkude pia alikataa wazo la kutolewa kwa mkopo kwenda Singida Black Stars FC, akisisitiza kwanza amalize suala la madai yake ili haki yake ipatikane.

Mashabiki wengi wa soka Tanzania wanaendelea kufuatilia kwa karibu sakata hili wakisubiri kuona Mkude atarejea lini tena dimbani.

Jonas Mkude

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons