Allan Okello akwama Uganda

Siku kadhaa zilizopita niliwataarifu hapa kuwa Allan Okello ataichezea timu yake ya mkoa wa Lango kwenye mchezo wa robo fainali ya mashindano ya FUFA Drum dhidi ya mkoa wa Teso.

Mchezo wenyewe ulichezwa jana na Allan Okello alishindwa kucheza kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu ya mkoa wake kupata ushindi wa bao 1-0.

Sababu za kutocheza kwake ni zuio kutoka kwa viongozi wa klabu yake, Young Africans.

Okello alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa timu yake ya mkoa hadi dakika za mwisho, lakini klabu yake ya Yanga SC haikumruhusu kucheza mchezo huo.

Yanga kwa sasa inakabiliwa na wimbi kubwa la majeruhi kwa wachezaji wake, hivyo hawakutaka kuchukua hatari yoyote ile.

Walihofia kwamba anaweza kuumia, hivyo wakamtaka arejee Dar Es Salaam Jumapili asubuhi.

Hata hivyo, Allan aliweza kuwashawishi wamruhusu kubaki na kuangalia mechi kama shabiki, lakini hawakumpa ruhusa ya kucheza.

Kwa hiyo Allan Okello hakucheza mchezo huo kutokana klabu ilitaka kumlinda ili abaki fiti kwa ajili ya mechi zao zijazo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI