MWANZO WA AFRIKA -2

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia 

UKOLONI

WAZUNGU walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika.

Endelea

Katika mwaka 1488 Bartolomeo Dio alizunguka rasi ya Tumaini Jema (kwa Kiingereza Cape of Good Hope) na katika mwaka 1498;Vasco da Gama alifika ufukwe wa Afrika mashariki na kuendelea mpaka India.

Baada ya hapo, Ureno ulianzisha vituo vya biashara Afrika, ukifuatiwa na Waholanzi, Waingereza, Wafaransa na Wazungu wengineo, na biashara ya watumwa iliyosimamiwa na Waarabu na baadhi ya Waafrika wenyewe ikashika kasi kwa nguvu.

Wakati huo huo Waturuki walishikilia sehemu za kaskazini ya Afrika na Waomani wakashikikia ufukwe wa Afrika mashariki.

Kati ya miaka ya 1880 na 1972 Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia.

Wafaransa wakachukuwa Afrika magharibi na kaskazini na Kwa hiyo nchi za Afrika magharibi Dahomey (sasa Benin), Guinea, Mali, Cote d' Ivoire, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya juu (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake.

Hali kadhalika, Algeria, Tunisia, Morocco, zilichukuliwa na wao, aidha Wafaransa walitawala Togoland, Swaziland, Madagascar, Comoro na Reunion.

Waingereza nao wakatawaka Afrika mashariki na kusini na kuwa sehemu ya Sudan na Somalia, Uganda, Kenya na baadaye Tanzania (chini ya jina la Tanganyika, Zanzibar) Nyasaland na Rhodesia.

Bechuanaland, Basutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika Kusini walitawala Transvaal, Orange Free Starr, Cape Colony, na Natal na huko Afrika ya magharibi walitawala Gambia, Sierra Leone, The Gold Coast na Nigeria.

Wareno wakachukuwa sehemu ya Guinea, Angola na Msumbiji na sehemu na visiwa fulani fulani huko Afrika ya magharibi.

Wabelgijibwakachukuwa Kongo na Rwanda- Urundi, na Wahispania wakachukuwa sehemu ya Guinea, Spanish Sahara (sasa Sahara magharibi) Ifn na sehemu za Morocco.

Wajerumani nao wakachukuwa Togoland, Cameroon na baadhi ya nchi katika Afrika ya magharibi na Afrika ya mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya dunia wakanyang' anywa.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons