Timu 10 za Afrika kombe la Dunia 2026

RASMI: Afrika itaenda kuwakilishwa na mataifa 10 kwenye fainali za kombe la dunia mwezi June pale Marekani, Mexico na Canada mara baada ya hii leo DR Congo kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamaica katika mchezo wa mchujo (Play-off).

Na hiyo inatokana na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Jamaica.

Katika mchezo huo wa hatua ya mchujo uliokuwa na ushindani mkali, bao la ushindi lilipatikana katika dakika ya 100 ya muda wa nyongeza kupitia kwa beki Axel Tuanzebe, aliyewahakikishia "The Leopards" nafasi hiyo adhimu.

​Hatua hii ni mafanikio makubwa kwa majirani zetu DR Congo, kwani inawafanya kuwa miongoni mwa wawakilishi wa bara la Afrika watakaopeperusha bendera katika fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada, na Mexico.

 Ushindi huo umepokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wa soka kote ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, wakisubiri kwa hamu kuona namna kikosi hicho chenye vipaji vingi kitakavyochuana na mataifa makubwa duniani kote. 




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons