Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2025

KMC yamnyooshea mkono wa kwaheri Maximo

Klabu ya KMC FC imefikiria kumpa mkono wa kwaheri kocha wao mkongwe Marcio Maximo, kutokana na mwendelezo mbovu klabuni humo. Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, zinasema kocha huyo tayari amepewa idadi ya michezo na watakaanae kikao kizito weekend hii endapo atapoteza mchezo wake dhidi ya Yanga kujua kuhusu kibalua chake. KMC FC wamekuwa na wakati mgumu kwenye Ligi msimu huu licha ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji lakini wamepoteza michezo yote iliyofuata na mpaka sasa wana alama tatu pekee wakiwa nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi hiyo.

Kocha wa Yanga aula Zambia

Aliyewahi kuwa kocha wa Young Africans,Noel Mwandila ameteuliwa kuwa kocha wa washambuliaji wa timu ya taifa ya Zambia ambayo kwa Sasa itakuwa chini ya kocha Moses Sichone ambaye anachukua nafasi ya Avram Grant aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni. Benchi kamili la timu ya taifa ya Zambia ambalo litasimamia timu AFCON nchini Morocco hili hapa, Kocha Mkuu: Moses Sichone Kocha Msaidizi wa Kwanza: Andrew Sinkala Kocha Msaidizi wa Pili: Perry Mutapa Kocha wa Magolikipa: Kennedy Mweene Kocha wa Mazoezi ya Viungo: Joseph Musonda Kocha wa Washambuliaji: Noel Mwandila

Stars hadharani, Kapombe, Tshabalala warejeshwa

KOCHA Muargentina, Miguel Angel Gamondi amewarejesha mabeki wakongwe, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Kuwait Ijumaa ya Novemba 14 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo nchini Misri. Wawili hao hawakuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichochapwa 2-0 na Iran Oktoba 14 kwenye mchezo mwingine wa kirafiki Uwanja wa Rashid, Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) chini ya kocha mzawa, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ aliyeondolewa baada ya kichapo hicho. TFF ilimtambulisha rasmi Gamondi November 4 kuwa kocha mpya wa Taifa Stars baada ya makubaliano na klabu yake, Singida Black Stars na kikosi chake kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili baada ya mechi za wikiendi za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara tayari kwa safari ya Misri.

MIGUEL GAMONDI ANAWEZA KUWA MWAROBAINI WA TAIFA STARS AFCON 2025

Na Prince Hoza Matua SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtambulisha Muargentina Miguel Angel Gamondi kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya wakubwa ‘Taifa Stars’ baada ya kuachana na mzawa, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’. Gamondi ataiongoza Tanzania kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Kuwait Ijumaa ya Novemba 14 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo nchini Misri. Ni wiki kocha huyo wa Singida Black Stars alipotangazwa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akichukua nafasi ya mzawa, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ aliyeondolewa. Gamondi amekitaja kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo baada ya mechi za wikiendi za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara tayari kwa safari ya Misri. TFF imechukua hatua hiyo ya kumfuta kazi Morocco na kumwajiri Gamondi ambaye mafanikio yake akiwa na klabu ya Yanga SC pamoja na Singida Black Stars tunayafahamu. Kocha huyo kipenzi cha wengi alijiunga na Yanga msimu juzi akichukua mikoba ya Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye naye aliiwezesha Yanga kufika...