WENYEJI, Mashujaa FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kwa matokeo hayo, Mashujaa FC wanafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya tatu wakizidiwa pointi moja na JKT Tanzania baada ya wote kucheza mechi nane — wakati Pamba Jiji FC pia ina pointi 12, lakini imecheza mechi saba.
Kwa upande wao Dodoma Jiji FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao sita za mechi nane sasa nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.
