Hali si shwari kabisa huko Ufaransa kwa mshambuliaji wa taifa la Tanzania na klabu yake ya Le Havre Mbwana Ally Samatta.
Samatta alisajiliwa na klabu ya Le Havre kama mchezaji huru August 5 mwaka huu baada ya mkataba wake na klabu ya Paok ya Ugiriki kutamatika.
Mpaka kufikia sasa Samatta hajafanikiwa kufunga bao hata moja wala kutoa pasi ya bao licha ya kuanza kwenye miche 8 kati 13 ya ligi ambayo klabu ya Le Havre imeshacheza.
Kwa sasa klabu ya Le Havre inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu baada kucheza za michezo 13,kushinda michezo 3,sare 5 na vipigo 5.
