Timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro imeifunga TRA United mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara.
Mabao ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Yusuph Chipo yamefungwa na Kassim Shaibu dakika ya 40 na Ismailia Mjesa dakika ya 90 wakati bao la kufutia machozi la TRA United limefungwa na Adam Adam dakika ya 13
