Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imemfungia mechi tatu na kumtoza faini ya dola za Kimarekanl 5,000 (sawa ba zaidi ya Milioni 12 za Kitanzania) winga wa klabu ya Al Hilal Omduman ya Sudan Girumugish kwa vitendo visivyo vya kiungwana michezoni kutokana na alichokifanya baada ya mchezo wa timu yake na Mc Alger uliopigwa Novemba 28 na kumalizika kwa Al hilal kiushinda bo 2-1.
Kutokana na adhabu hiyo, Girumugisha ataikosa michezo hii:
• vs St Eloi Lupopo
• vs Mamelodi Sundowns
• vs Mamelodi Sundowns
Caf waneweka wazi madai ya nyota huyo kurusha chupa kwenye benchi la Mc Alger sio miongoni mwa vitendo vilivyoainishwa kama ilivyokuwa ikieleza awali.
