Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Logo ya Simba Sports Club haitambuliki kisheria hii ambayo inatumika sasa maana ni tofauti na iliyosajiliwa, Ofisi ya AG inashauri Klabu isajili logo ya sasa maana Mtu akiitumia vinginevyo hakuna uhalali wa kumtia hatiani kisheria itakuwa ngumu na klabu inaweza kupoteza haki zake.
Yaani kiufundi Mtu akitumia logo ya sasa kuzalisha chochote sio kosa maana haipo kisheria.
Hata Logo zilizosajiliwa zilitakiwa kuwa zimehuishwa kabla ya tarehe 4 Novemba, 2017. Inashauriwa Alama hizo zihuishwe ili kuondokana na hatari ya kufutwa kutoka katika Rejista ya Msajili wa Alama za Biashara na Huduma(BRELA) kwa mujibu wa Kanuni ya 54 – 55 ya Kanuni za Alama za Biashara na Huduma za Mwaka 2000.
