Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC, usiku huu imepoteza mchezo mwingine baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Wydad Athletic ya Morocco uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.
Bao pekee la Wydad Athletic limefungwa na Nordin Amrabat dakika ya 56, huu ni mchezo wa pili kwa Azam FC kupoteza baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wake wa kwanza uliofanyika ugenini.
