"Stade Malien walivuna alama moja lakini Esperance walikuwa bora zaidi kwenye mchezo baina yao, na walipoteza nafasi nyingi sana hivyo nadhani Esperance wana ubora wa juu kuliko Malien.
Malien wana wachezaji wazuri, lakini mara nyingi wanahusudu matumizi makubwa na kucheza soka la kushambulia moja kwa moja (direct football), hivyo nadhani tuna nafasi.
Sisi tuna timu bora zaidi na tuna wachezaji bora ukilinganisha na Stade Malien, tuna wachezaji wazuri kwenye kila eneo
Nadhani kwetu sio changamoto kwenda kucheza kwao, kwa sababu uwanja wao una sehemu kubwa ya kuchezea na mzuri hivyo tunaweza kucheza aina yetu ya soka. Na tunachohitaji ni kufunga tu.."
-Dimitarantev, Meneja wa Simba SC
