Ni mchezo wa pili katika hili kundi gumu zaidi, tumefanikiwa kupata pointi 3 za kwanza nyumbani na kesho tuna mechi nyingine ngumu hapa dhidi ya JS Kabylie.
“Ni mpinzani mgumu sana na ana nguvu kubwa ya mashabiki. Hii ni mara yangu ya nne nakuja hapa Algeria kuwaona JS Kabilie. Ni Klabu yenye hamasa na mashabiki wengi sana”
“Kwetu Yanga ni mazingira mazuri kuwepo hapa, kucheza dhidi ya Klabu mbele mbele ya mashabiki wengi pia uwanjani, tumekuja kupambana kupata pointi 3 hapa na sio kitu kingine.”
