Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Barcelona na Vilabu vingine mbalimbali ulimwenguni Samuel Eto’o Fils (44), amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT) kwa mara ya pili mfululizo.
Katika Mkutano wa Uchaguzi mkuu uliofanyika huko Mbankomo eneo la kati la Cameroon karibu na mji mkuu wa Yaoundé,amechaguliwa kwa kura 85 kati 87 ambapo kura mbili zimeharibika.
Eto’o alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza FECAFOOT mnamo Desemba 2021.
Mchakato wa Uchaguzi umekabiliwa na mvutano wa kisiasa huku Wizara ya Michezo ikijaribu kusimamisha Uchaguzi huo hapo awali lakini FECAFOOT ukasisitiza kwamba taratibu zake zinafuata kanuni za Kimataifa za Mpira wa Miguu.
Wagombea wengine wawili Yianick Heumo Leudjeu na Georges Kalgong waliondolewa kwenye mchakato huo na kumuacha Eto’o akiwa Mgombea pekee.
