Balozi wa Tanzania nchini Mali ambaye makazi yake yapo Abuja, Nigeria, Selestine Gervas Kakele, ametembelea mazoezi ya Simba SC, leo Novemba 28, uwanja wa Lafia Club De Bamako, mjini Bamako kwa ajili ya kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa Jumapili wa kundi “D” Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien.
Balozi Kakele amewatia moyo wachezaji na kuwasisitiza kwamba, mchezo wa kwanza waliopoteza nyumbani dhidi ya Petro Atletico ya Angola ulishapita, sasa vita ni dhidi ya Stade Malien na imani yake timu itapata ushindi.
Simba ipo Mali kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Stade Malien Jumapili ya Novemba 30, saa 1:00 usiku





