Na Prince Hoza Matua
TANGU msimu wa 2025/2026 wa michuano ya CAF ilipoanza na Simba SC kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika na kwa jitihada zake ikafanikiwa kutinga hatua ya makundi.
Haikuwa rahisi Simba SC ilianzia raundi ya awali na ilipangwa kukutana na klabu ya Gaborone United ya Botswana ambapo ilianzia ugenini, Wekundu wa Msimbazi, walisafiri hadi mjini Gaborone na kukutana na miamba hiyo ya Gaborone United.
Simba ilikuwa ikinolewa na kocha wake Fadlu David's raia wa Afrika Kusini na iliingia kwenye mchezo huo huku kukiwa na tetesi kwamba kocha wake mkuu Fadlu anataka kubwaga manyanga.
Na ilidaiwa kwamba kocha huyo ataaga baada ya mchezo huo, kuna mambo mengi yameibuka ndani ya klabu hiyo ingawa tulijua kama tetesi tu yanasemwa mchana na usiku watalala, lakini Simba katika mchezo huo iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Baadaye Fadlu alibwaga manyanga na kutimkia klabu yake ya zamani ya Raja Athletic Club ya Morocco, ikabidi Simba irejee Dar es Salaam bila kocha wake mkuu kwani hata kocha msaidizi Seleman Matola naye alikumbwa na adhabu.
Katika mchezo dhidi ya Gaborone United, Matola alioneshwa kadi nyekundu hivyo alishindwa kusimama kwenye mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam, uongozi wa Simba ilibidi ufanye mazungumzo na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Hemed Morocco Ili asimame katika touch line kwenye mchezo dhidi ya Gaborone United.
Morocco licha ya kuwa kocha wa Taifa Stars, lakini alienda kuisaidia Simba na kuiongoza katika mchezo huo wa marudiano dhidi ya Gaborone United na Simba kutinga hatua ya makundi baada ya sare ya kufungana bao 1-1.
Hata hivyo makubaliano ya Simba na Morocco yalikuwa ya mechi moja na Simba ilianza mchakato wa kutafuta kocha mpya, Dimitar Pantev raia wa Burgalia aliajiriwa na Simba kuwa kocha mkuu.
Leseni yake ya UEFA ilimfanya awe meneja mkuu badala ya kocha mkuu pale Simba inapocheza mechi za ligi za nyumbani lakini anakuwa kocha mkuu kwenye mechi za CAF.
Simba waliridhishwa na aina ya ufundishaji wake akiwa na klabu ya Gaborone United ambapo Simba ilipata tabu sana kuitoa timu hiyo kwenye mchezo wake wa raundi ya awali zilipokutana, Pantev ni kocha mwenye mikakati mikubwa na soka lake ni la kuvutia.
Mashabiki wa Simba wenyewe walifurahishwa na ujio wake, ni mburudishaji mzuri akiwa na timu yake ndani ya uwanja, na pia ana mbinu za kupata mabao, alianza mchezo wake dhidi ya Nsingizini Hotspurs ambapo Simba ilicheza ugenini na ikishinda mabao 3-0.
Anapendelea sana kutumia mshambuliaji kizuri yaani namba tisa wa uongo, alianza na Kibu Denis dhidi ya Nsingizini Hotspurs na Simba ikishinda 3-0 ambapo Kibu alifunga mabao mawili, na moja alifunga beki wa kati Wilson Nangu.
Simba imeanza kubadilika na mwenendo wake umekuwa mzuri ingawa msimu huu haijaweza kupata ushindi katika uwanja wa Mkapa, ikiwa chini ya Morocco Simba ilipata sare na Gaborone United 1-1 na chini ya Pantev ikapata sare ya 0-0 na Nsingizini Hotspurs.
Kufungwa 1-0 dhidi ya Petro de Luanda ya Angola hatua ya makundi zilipeleka lawama za wazi wazi kwa Pantev na akionekana si lolote si chochote, Pantev anaonekana si kocha kwa sababu hajamwazisha mshambuliaji halisi anayesimama mbele.
Kocha huyo amemtumia Elie Mpanzu kama mshambuliaji kivuli, mashabiki wa Simba wamemkataa na pia kila mmoja amegeuka mchambuzi akimkataa zaidi, kiukweli mimi binafsi nasema ni bonge la kocha kwani kuna kitu nakiona ndani ya Simba.
Kama akiendelea kuinoa timu hiyo ninaamini itakuwa timu tishio barani Afrika, licha kwamba amekuta wachezaji ambao sio bora sana, lakini ataibadili na kuijenga na hatimaye itakuwa timu tishio.
ALAMSIKI
