Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2023

SIMBA WAKABIDHI MAHITAJI MUHIMU SHULE YA MSINGI SINZA MAALUM

Picha
Simba SC leo wametembelea Shule ya Msingi Sinza Maalum na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinaadamu kama ambavyo tunafanya kila mwaka. Kila inapofika wiki ya Simba mpaka kufika kilele chake cha Simba Day huwa tunakuwa na matukio mbalimbali ya kurejesha kwa jamii.

BAKARI SHIME ACHAFUA HALI YA HEWA ZANZIBAR

Picha
Mchambuzi Kheir Salum kupitia Asubuhi Njema ya ZBC, amesema kauli iliyotolewa kocha wa timu ya wanawake ya Tanzania Bara U18, Bakari Shime baada ya mchezo wa CECAFA uliopigwa siku ya jana dhidi ya timu ya Wanawake Zanzibar U18 kuwa timu hiyo iliingia kwenye mchezo kwa lengo la kuvuruga tu kwa kuwa wanajua wao wako chini kisoka mbele ya Bara. Kheir amesema kauli hiyo si ya kiungwana na kama Mwalimu ilipaswa awaheshimu wapinzani wake.

JEZI YA SPIKA WA BUNGE YAUZWA MIL 2.5

Picha
Jezi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Tawi la Simba Makini katika Mnada unaoendelea katika Ofisi za Azam TV.

MESSI AIGALAGAZA TP MAZEMBE, SASA KULIPWA MAMILIONI

Picha
Ramadhan Singano ameshinda kesi yake dhidi ya TP Mazembe kuhusu malipo yake ya signing fee, ukiukwaji wa vifungu vya kimkataba na mishahara yake, alipata ushindi FIFA ila Mazembe wakaenda CAS ambapo wamebwagwa tena, wanapaswa kumlipa Kijana ndani ya siku 35. Singano alikuwa na Wanasheria wawili wa kimataifa, kutoka Kenya na Venezuela ambao ndio walisimama kwenye mapambano kwa zaidi ya miaka miwili ya kesi hiyo dhidi ya miamba Mazembe. Kwa sasa rasmi yupo huru ana aweza kujiunga na timu yoyote ile!

KIPA WA ZALAN KUTUA SIMBA

Picha
Taarifa za chini ya kapeti zimethibitisha kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo kwenye mpango wa kuinasa saini ya mlinda lango wa klabu ya Zalan Fc, Majok Majok (21), Uongozi wa klabu ya Simba umeridhia kuanza mchakato wa kuipata saini ya Mlinda lango huyo kwa haraka zaidi ili kuja Tanzania kuvaa viatu vya Mbrazil Luis Jefferson aliyeachwa kikosini kutokana na kutokidhi vigezo vya mchezaji wa kigeni anayetakiwa kucheza Ligi Kuu Tanzania, Kwa sasa itawalazimu Simba Sc kusajili mlinda lango huku wakilipa na faini kutokana na kusajili nje ya muda wa dirisha la kawaida.

RASMI, KIPA MBRAZIL WA SIMBA NJE MIEZI 6

Picha
"Ni kweli amepata changamoto, ni kweli kama unavyosema huwa tunawapima Wachezaji, lakini kumbuka Kuumia si jambo la mchakato ni jambo la mara moja" "Alikuja mzima kabisa lakini ameumia mazoezini, na atakaa nje kwa zaidi ya miezi (6). Tutatoa taarifa kuwajuza, tuko tunapambana kutafuta golikipa mwingine"

TRY AGAIN ATEMBELEA KAMBI YA SIMBA HUKO UTURUKI

Picha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Muhene ‘Try Again’ ametembelea kambi ya timu ya Simba hapa jijini Ankara, Uturuki ambapo amepata nafasi ya kuongea na wachezaji na benchi la ufundi mambo mbalimbali kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

MORRISON ANATAKA MSHAHARA MKUBWA ASAINI SINGIDA FOUNTAIN GATE

Picha
Kikao kinaendelea Dar es Salaam, Tanzania kati ya Uongozi wa Singida Fountain Gate na winga Bernard Morrison juu ya uwezekano wa kuipata saini ya Mchezaji huyo. Morrison anahitaji mshahara mkubwa sana, issue ni maslahi binafsi, ila kuna uwezekano wa Bernard Morrison akajiunga na Singida Fountain Gate.

ISSA NDALA KUTUPIWA VIRAGO AZAM FC

Picha
Baada ya usajili wa kiungo Mkongoman Yanick Bangala kukamilika pale Azam FC, habari zinasema kwamba kiungo kutoka Nigeria Issa Aliyu Ndala atapewa Thank you hivi karibuni klabuni hapo kwakuwa Azam tayari walikuwa na wachezaji 12. Azam hivi karibuni imeachana na kiungo mshambuliaji wake Tape Edinho kutoka Ivory Coast ambaye Kama ilivyo kwa Ndala alishajiliwa msimu uliopita lakini akatolewa kwa mkopo. Tape ameachwa ili kutii kanuni ya Ligi kuu inayotaka vilabu kuwa na wachezaji wa kigeni 12, Azam wao wakawa wako 13 ndipo Tape akaonyeshwa mlango wa kutokea. Ndala sio chaguo la kwanza la kocha Yousouf Dabo kutoka Senegal. Dabo yeye anawapa chaguo la kwanza Sospeter Bajana, James Akaminko na Feisal Salum eneo la kiungo kwahiyo haikuwa kazi ngumu kumkata Ndala na kumleta Bangala ambaye anacheza pia kama beki wa kati ambako mpaka sasa Dabo anaonekana kuwapa nafasi kubwa Edward Manyama na Malick Ndoye huku Daniel Amoah kutoka Ghana akupe kama chaguo la pili.

MAYELE ATAMBULISHWA PYRAMIDS

Picha
Klabu ya FC Pyramids imetangaza kukamilisha Usajili wa aliyekuwa Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Yanga SC, Fiston Mayele kwa Mkataba wa Miaka mitatu. Mayele mwenye umri wa Miaka 29 ameuzwa na Yanga SC baada ya kuwapa Mafanikio makubwa Klabu hiyo ya Tanzania. .

SIMBA SASA KUSHUSHA KIPA MWINGINE TOKA NIGERIA

Picha
Vita ya Kuipata saini ya Mlinda lango raia wa Nigeria John Noble (30) imefikia pazuri kwakuwa Klabu ya Kitayosce kutoka Tabora ilishazungumza na kilichosalia ni kusaini Mkataba huku klabu ya Simba nayo Ikiongeza Ushawishi kwake wa Maslahi ili aendelee kwao (Simba Sc), Imefahamika kuwa Mlinda lango huyo ambaye amemaliza mkataba na waajiri wake Enyimba (Free Agent) ana nafasi kubwa kutangazwa ndani ya Simba Sc kabla dirisha la usajili la CAF kufungwa, Muda wowote kuanzia sasa Uongozi wa klab ya Simba Utatangaza kuachana na Mlinda lake aliyedumu kwa muda mfupi zaidi (raia wa Brazil Luis Jefferson) baada ya kutokuwa na Vigezo vya kuchezea klabu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara (NBC).

SIMBA KUREJEA AGOSTI 2

Picha
Kikosi cha Simba SC kinatarajia kurejea nchini Agosti 2 kuelekea na maandalizi ya mwisho kuingia msimu mpya wa 2023/24 ikiambatana mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day pamoja na michezo ya Ngao ya Jamii itakayochezwa CCM Mkwakwani, Tanga. Simba SC itacheza mchezo wa mwisho wa kirafiki wakiwa nchini Uturuki leo saa kumi na mbili jioni baada ya hapo wataendelea na program za mazoezi pekee kabla ya kurejea nchini.

KIPA MBRAZIL WA SIMBA YADAIWA NI MAJERUHI WA MARA KWA MARA

Picha
Inasemekana Mlinda mlango mpya wa klabu ya Simba Jefferson Luis raia wa Brazil ana majeraha ya muda mrefu hivyo inadaiwa atashindwa kusimama imara kwenye lango la timu hiyo. Simba imeamua kumsajili Luis ili atumike kwenye michuano ya ndani na kimataifa kwa sababu kipa wake chaguo la kwanza Aishi Manula amepewa mapumziko ya miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini. Kitendo cha Manula kukaa nje miezi minne inabidi klabu ya Simba itafute kipa mwingine kwani Ally Salim ambaye ni kipa chaguo la tatu kushindwa kukaa langoni kwa umahiri, Luis inasemekana ana majeraha ya mara kwa mara hivyo anaweza kuigharimu timu

Rasmi Sadio Mane amfuata Ronaldo

Picha
Sadio Mane amekamilisha usajili wake kujiunga na klabu ya Al Nassr kutoka Saudia kuelekea msimu ujao. Bayern Munich wamemalizana na Al Nassr kuhusu malipo ya uhamisho huo, kilichosalia ni vipimo vya afya ambavyo wiki ijayo vitafanyika ili kukamilisha dili hilo.

CEO AZAM FC ATEMBELEA KWA MAN UNITED, CITY NA SPURS KUJIFUNZA

Picha
Mara baada ya kumaliza zoezi la usajili, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim.Amin "Popat", ametua Makao Makuu wa Manchester United kwa ziara maalum ya kujifunza. CEO Abdulkarim Amin, ametinga kwa miamba hiyo ya England, akiwa amevalia uzi mpya bora na wa viwango wa Azam FC. Mbali na kufanya ziara ndani ya viunga vya Old Trafford kwa wababe hao wa jiji la Manchester, pia atatembelea kwa mabingwa wa EPL na UEFA, Man City na Totenhan Spurs lengo likiwa ni kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo soka kutoka kwa miamba hiyo.

Mjue Gift Fred, beki mpya wa kati aliyechukua nafasi ya Mamadou Doumbia

Picha
Na Salum Fikiri Jr MIAKA kadhaa iliyopita Yanga SC lilikuwa jina kubwa nchini Uganda hasa kwa sababu ilizoeleka mara kwa mara kwenda kucheza na timu za huko na pia kusajili wachezaji mbalimbali.  Ikumbukwe mwaka 1993 na 1999 Yanga ilienda kushinda ubingwa wa Klabu biogwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame, Yanga iliweza kusajili nyota mbalimbali nchini Uganda kama Hamisi Kiiza "Diego" ambao walitokea kujipatia umaarufu mkubwa.  Yanga ikapotea machoni mwa Uganda na likabaki jina tu ambalo linaendelea kusikika pande mbalimbali za Afrika na dunia, umaarufu wa Yanga unatokana na na uwezo wake uliouonyesha msimu uliopita ambapo iliweza kufika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, pia iliweza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu bara na mengineyo.  Ingawa tayari ina mchezaji kutoka Uganda Khalid Aucho, ikitaka kujiimarisha zaidi ili kushindana ndani na nje ya nchi. Kikubwa wanachokiangalia Yanga ni kufika makundi Ligi ya mabingwa barani Afrika. Baada ya msimu uliopit...

CARLOS PROTUS AREJEA LIGI KUU BARA

Picha
Klabu ya Geita Gold imekamilisha usajili wa Beki wa Kimataifa wa Tanzania,Carlos Protus akitokea Klabu ya Tusker ya Kenya. Carlos anakuwa Mchezaji wa nne kutangazwa na Geita Gold baada ya Tariq Kiakala aliyetokea Mbeya City, Yusuph Dunia akitokea Kagera Sugar na Valentino Mashaka akitokea Ruvu Shooting.

WAKAGUZI WA MIUNDOMBINU WA CAF WAWASILI DAR

Picha
Wakaguzi wa Miundombinu wa CAF kwa ajili ya uwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika 2027 wakifanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Terminal II, Dar es Salaam

MRITHI WA MGUNDA MBIONI KUTUA SIMBA

Picha
Aliyekuwa kocha msaidizi wa kocha Robertinho kipindi wakiwa ndani ya klabu ya Vipers ya Uganda Marcelo Cardoso, anatua Simba sc kuvaa Viatu vya Juma Mgunda, Taarifa zinathibitisha kuwa Marcelo ndio kocha Msaidizi wa kikosi wa Simba baada ya Mazungumzo ya pande zote mbili kwenda sawa.

KONKANI AJIUNGA NA YANGA

Picha
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Ghana Hafidh Konkani kwa Mkataba wa miaka miwili. Konkani (23) akiwa na Benchem Utd msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 15 katika Ligi Kuu ya Ghana. Mfungaji namba mbili wa ligi kuu ya Ghana anamiaka (23) Mechi 27 Goal 15 Assist 4 Anacheza timu ya taifa ya Ghana

ROMA AMKANA NEY WA MITEGO

Picha
Msanii wa Hip Hop, Roma amelitaka Baraza la Taifa (Basata) kumbana Nay wa Mitego yeye mwenyewe kuhusu wimbo wake mpya, Amkeni. Kauli ya Roma inakuja baada ya Nay kudai baadhi ya mistari ya wimbo huo alipatiwa na Roma kitu ambacho amekikanusha. "Sijamtumia kitu chochote wala sijahusika kwenye wimbo wake huo, kwanza hata namba yake ya simu sina, ananisingizia na sijapenda!." "Akija hiyo Jumatatu, malizaneni naye pekee yake, mimi nina familia na watoto wananitegema kupitia huu muziki, sitaki hekaheka sasa hivi." ameandika Roma.

WAISLAMU NIGERIA WAMJIA JUU MCHEZAJI WA TIMU YA WANAWAKE KUVUA JEZI

Picha
Waumini wa Dini ya kiislamu nchini Nigeria wamelani kitendo cha Mchezaji wa Timu ya Taifa Nigeria Asisat Oshoala baada ya kuvua jezi wakati anashangilia goli alilolifunga dhidi ya Australia kuwa ni kinyume na dini yao. Waislamu hao wameomba FIFA waifute video hiyo na timu ya Taifa ya Nigeria wapokonywe point 3 na wapewe timu ya Taifa ya Australia. .