ISSA NDALA KUTUPIWA VIRAGO AZAM FC
Baada ya usajili wa kiungo Mkongoman Yanick Bangala kukamilika pale Azam FC, habari zinasema kwamba kiungo kutoka Nigeria Issa Aliyu Ndala atapewa Thank you hivi karibuni klabuni hapo kwakuwa Azam tayari walikuwa na wachezaji 12.
Azam hivi karibuni imeachana na kiungo mshambuliaji wake Tape Edinho kutoka Ivory Coast ambaye Kama ilivyo kwa Ndala alishajiliwa msimu uliopita lakini akatolewa kwa mkopo.
Tape ameachwa ili kutii kanuni ya Ligi kuu inayotaka vilabu kuwa na wachezaji wa kigeni 12, Azam wao wakawa wako 13 ndipo Tape akaonyeshwa mlango wa kutokea.
Ndala sio chaguo la kwanza la kocha Yousouf Dabo kutoka Senegal. Dabo yeye anawapa chaguo la kwanza Sospeter Bajana, James Akaminko na Feisal Salum eneo la kiungo kwahiyo haikuwa kazi ngumu kumkata Ndala na kumleta Bangala ambaye anacheza pia kama beki wa kati ambako mpaka sasa Dabo anaonekana kuwapa nafasi kubwa Edward Manyama na Malick Ndoye huku Daniel Amoah kutoka Ghana akupe kama chaguo la pili.