MESSI AIGALAGAZA TP MAZEMBE, SASA KULIPWA MAMILIONI
Ramadhan Singano ameshinda kesi yake dhidi ya TP Mazembe kuhusu malipo yake ya signing fee, ukiukwaji wa vifungu vya kimkataba na mishahara yake, alipata ushindi FIFA ila Mazembe wakaenda CAS ambapo wamebwagwa tena, wanapaswa kumlipa Kijana ndani ya siku 35.
Singano alikuwa na Wanasheria wawili wa kimataifa, kutoka Kenya na Venezuela ambao ndio walisimama kwenye mapambano kwa zaidi ya miaka miwili ya kesi hiyo dhidi ya miamba Mazembe.
Kwa sasa rasmi yupo huru ana aweza kujiunga na timu yoyote ile!