SIMBA SASA KUSHUSHA KIPA MWINGINE TOKA NIGERIA
Vita ya Kuipata saini ya Mlinda lango raia wa Nigeria John Noble (30) imefikia pazuri kwakuwa Klabu ya Kitayosce kutoka Tabora ilishazungumza na kilichosalia ni kusaini Mkataba huku klabu ya Simba nayo Ikiongeza Ushawishi kwake wa Maslahi ili aendelee kwao (Simba Sc),
Imefahamika kuwa Mlinda lango huyo ambaye amemaliza mkataba na waajiri wake Enyimba (Free Agent) ana nafasi kubwa kutangazwa ndani ya Simba Sc kabla dirisha la usajili la CAF kufungwa,
Muda wowote kuanzia sasa Uongozi wa klab ya Simba Utatangaza kuachana na Mlinda lake aliyedumu kwa muda mfupi zaidi (raia wa Brazil Luis Jefferson) baada ya kutokuwa na Vigezo vya kuchezea klabu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara (NBC).