KIPA MBRAZIL WA SIMBA YADAIWA NI MAJERUHI WA MARA KWA MARA

Inasemekana Mlinda mlango mpya wa klabu ya Simba Jefferson Luis raia wa Brazil ana majeraha ya muda mrefu hivyo inadaiwa atashindwa kusimama imara kwenye lango la timu hiyo.

Simba imeamua kumsajili Luis ili atumike kwenye michuano ya ndani na kimataifa kwa sababu kipa wake chaguo la kwanza Aishi Manula amepewa mapumziko ya miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

Kitendo cha Manula kukaa nje miezi minne inabidi klabu ya Simba itafute kipa mwingine kwani Ally Salim ambaye ni kipa chaguo la tatu kushindwa kukaa langoni kwa umahiri, Luis inasemekana ana majeraha ya mara kwa mara hivyo anaweza kuigharimu timu


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA