BAKARI SHIME ACHAFUA HALI YA HEWA ZANZIBAR
Mchambuzi Kheir Salum kupitia Asubuhi Njema ya ZBC, amesema kauli iliyotolewa kocha wa timu ya wanawake ya Tanzania Bara U18, Bakari Shime baada ya mchezo wa CECAFA uliopigwa siku ya jana dhidi ya timu ya Wanawake Zanzibar U18 kuwa timu hiyo iliingia kwenye mchezo kwa lengo la kuvuruga tu kwa kuwa wanajua wao wako chini kisoka mbele ya Bara.
Kheir amesema kauli hiyo si ya kiungwana na kama Mwalimu ilipaswa awaheshimu wapinzani wake.