ROMA AMKANA NEY WA MITEGO
Msanii wa Hip Hop, Roma amelitaka Baraza la Taifa (Basata) kumbana Nay wa Mitego yeye mwenyewe kuhusu wimbo wake mpya, Amkeni.
Kauli ya Roma inakuja baada ya Nay kudai baadhi ya mistari ya wimbo huo alipatiwa na Roma kitu ambacho amekikanusha.
"Sijamtumia kitu chochote wala sijahusika kwenye wimbo wake huo, kwanza hata namba yake ya simu sina, ananisingizia na sijapenda!."
"Akija hiyo Jumatatu, malizaneni naye pekee yake, mimi nina familia na watoto wananitegema kupitia huu muziki, sitaki hekaheka sasa hivi." ameandika Roma.