CARLOS PROTUS AREJEA LIGI KUU BARA
Klabu ya Geita Gold imekamilisha usajili wa Beki wa Kimataifa wa Tanzania,Carlos Protus akitokea Klabu ya Tusker ya Kenya.
Carlos anakuwa Mchezaji wa nne kutangazwa na Geita Gold baada ya Tariq Kiakala aliyetokea Mbeya City, Yusuph Dunia akitokea Kagera Sugar na Valentino Mashaka akitokea Ruvu Shooting.