Mkata umeme wa Lupopo kutua Simba
Tayari mabosi wa klabu ya Simba wamepiga hodi katika klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kumuulizia mkata umeme mmoja anayekipiga timu hiyo fundi wa mpira, Harvy Ossete ambaye juzi kacheza dakika 90 wakati chama lake la Congo likiibuka na ushindi katika mechi za kufuzu AFCON.
.
Ossete ambaye ni raia wa Congo , anatajwa kuwa kati ya viungo wanaotazamwa kwa sifa ambazo Robertinho anazihitaji kikosini, akiwa na uwezo wa kukaba, anachezesha timu na anaweza kucheza kama beki wa kati akihitajika japo si eneo lake halisi.