BARCELONA KUMRUDISHA MESSI
Klabu ya Barcelona kupitia kwa Makamu wake wa Rais, Rafael Yuste amekiri kuwa wapo katika mipango ya kumrejesha mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi kwenye klabu hiyo kutokea PSG.
Yuste amesema wao (Barcelona) wamekuwa na mawasiliano ya karibu na wawakilishi wa Lionel Messi na kwamba hata yeye (Messi) anafahamu kwa jinsi gani Barcelona wanampenda na wangependa arudi.
Unadhani itawezekana tena kwa Messi kurejea Barcelona?