Makala; Yanga imeweka historia Afrika

NA ABDUL MAKAMBO
Call. 0787905328. 

TAREHE 19-3-2023 siku ya Jumapili, tarehe na mwaka wa kihistoria kwa klabu ya Dar Young Africans au Yanga iliifunga wawakilishi wa Tunisia us Monastir magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkapa jijini.

Kwa hakika Yanga imeleta furaha kubwa kwa wanachama, wapenzi na heshima kubwa kwa taifa la Tanzania.

Ni baada ya miaka mingi-Yanga iliingia robo fainali kwa mara ya kwanza na ilikuwa ni michuano ya Klabu bingwa barani Afrika mwaka 1969 kule Addis Ababa kule nchini Ethiopia na Yanga ikatolewa kwa shilingi.



2.Tokea mwaka ule yanga haikufanya tena vizuri na mwaka 1998 yanga ndipo ilipofanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani afrika-ilicheza na apr ya rwanda ikaitoa na ikacheza na coffe ya ethiopia na ikaitoa na yanga ikaingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani afrika.Na kwenye makundi ilikua kundi moja na raja casablanca ya moroco.

Asec Mimosas ya Ivory Coast na Maning Rangers ya Afrika Kusini na Yanga ilikuwa chini ya kocha Tito Mwaluvanda na akaletwa Raoul Shungu raia wa DRC.

Na Yanga ilipata bahati nyingine tena mwaka 2016 Yanga ikiwa chini ya mfadhili Yusufu Mehboub Manji na kocha Mholanzi Hans Pluijm.

Na ilicheza Klabu bingwa na Gelgada Esperanca ya Angola na ilicheza na Al Ahry ya Misri.

Na Yanga iliangukia kwenye michuano ya Shirikisho Afrika.Ikicheza na Medeama ya Ghana, Mo Boejaia ya Algeria na Rayon ya Rwanda.

Natoka miaka hiyo Yanga haijafanya vizuri kwenye Klabu bingwa na hata kombe la Shirikisho.

Lakini ujio wa kocha Mtunisia Nasreddin Mohamed Nabi umekuwa ni mwanzo mzuri na bora kwa klabu ya Yanga na uwepo wa ufadhili GSM ni moja ya neema kwa klabu ya Yanga.

Nabi ni kocha mwenye falsafa  nzuri, kwa mafanikio  ya Yanga kuingia robo fainali ya Shirikisho Afrika italeta maendeleo na mafanikio makubwa ndani ya klabu ya Yanga.

Nabi leo ameweza kuwainua viwango akina Feisal Sakum au Feitoto, Fiston Mayele, Djuma Shaban, Joyce Lomalisa Mutambala, Farid Mussa na Clement Francis Mzize.



Kwa kweli wamepanda na wamebadilika kisoka na yote ni maelekezo na falsafa ya kimbinu ya kocha Nabi.

Kwa hakika Yanga imefanya makubwa na kocha Nabi atawapeleka mbali itachanua zaidi kwenye mashindano ya kimataifa.pongezi ziwaendee mlinda mlango Djigui Diarra Yanick Bangala, Khalid Aucho, Stephano Aziz Ki na Kennedy Musonda na wengineo.
Asanteni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA