SIMBA WAIANZA SAFARI YA MOROCCO 🚀
Baada ya jana kushindwa kusafiri kutokana na ndege iliyopangwa kusafiria kupata hitilafu,hii leo asubuhi kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca ambao utapigwa Jumamosi ya April 1,2023 kuanzia saa saba kamili usiku kwa majira ya Tanzania.
Simba wanatarajia kufika hii leo nchini Morocco lakini watapita Qatari kabla ya kuunganisha safari hadi Morocco wachezaji waliokwenye Mataifa yao wanatarajia kutokea kwenye mataifa yao hadi Morocco