Alikiba alia na mwtumizi makubwa ya kuandaa video
Staa wa mziki nchini @officialalikiba amesema video zinamaliza pesa nyingi kwa wasanii tofauti na audio ambazo zinaingiza pesa bila shida yoyote.
"Ni kweli tunafanya video lakini ukweli video inachukua pesa nyingi sana kwa wasanii na wanasubiri pesa zirudi. Unajua mziki ni biashara maono yangu nimejaribu kufanya mwaka huu 'Lyrics Video' ili waone reaction yangu nilivyoimba na kudeliver mziki wangu kupitia lyrics or dancing video".
"Wasanii wamekuwa wakipoteza pesa bila kujijua hiyo tafiti nimeifanya baada ya kutoa ' The Only One King' kuna video ambazo zimeingiza pesa zingine hazikuingiza pesa lakini audio ina penetrate na kuingiza pesa bila shida yoyote".