Simba kulipiza kisasi kwa Raja au kushindiliwa magoli?
Na Prince Hoza
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC usiku mnene itashuka dimbani saa 7:00 ya tarehe 1-4.2023 itarudiana na Raja Casablanca mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Simba ikiwa ugenini itakuwa na kazi ngumu kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 3-0 nyumbani katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Hivyo katika mchezo huo Simba inatakiwa kushinda ili kulipa kisasi, lakini vile vile inaweza kufungwa zaidi ya magoli 3 kwani itacheza mbele ya mashabiki wake.
Simba ina kumbukumbu nzuri hivi karibuni iliifunga timu ya Horoya ya Guinnea mabao 7-0 ushindi ambao umeshitua Afrika nzima kwani imepata tiketi ya kuingia robo fainali