Bilionea kuinunua Man United

Bilionea kutokea England Sir Jim Radcliffe na Kampuni yake ya kemikali INEOS wametuma tena zabuni nyingine iliyoboreshwa kwa ajili ya kuinunua klabu ya Manchester United.

Sheikh Jassim bin Hamad wa Qatar na Sir Jim Radcliffe wote waliwasilisha maombi ya kuhitaji muda zaidi wa kuyapangilia vizuri zaidi maombi yao.

Ujumbe kutokea kampuni ya INEOS wiki iliyopita uliitembelea klabu hiyo na kufanya mazungumzo ya saa sita vilevile ulipata wasaa wa kuvitembelea viwanja vya Old Trafford na Carrington. Nao ujumbe kutokea Qatar ulitembelea klabu hiyo na kufanya mazungumzo kwa saa kumi.

Wakati huohuo, Manchester United imetupilia mbali zabuni ya Mfanyabiashara wa Finland Thomas Zilliacus aliyekuwa na nia ya kuinunua klabu hiyo na kumiliki asilimia 50 huku akiiacha nusu nyingine imilikiwe na mashabiki.

Klabu hiyo inayomilikiwa na familia ya Glazer iko sokoni tangu mwaka jana . Uamuzi huo umekuja baada ya miaka mingi ya malalamiko na kutoridhishwa kwa mashabiki juu ya umiliki wa klabu hiyo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA