Mayele amfunika Chama
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga SC Fiston Mayele Hapo Jana kwenye timu yake ya taifa ya DR Congo alicheza kwa dakika 32 akitokea sub akichukua nafasi ya mshambuliaji wa klabu ya Sochaux inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Nchini Ufaransa,Aldo Kalulu.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya goli 1-1 ambapo DR Congo ilikuwa ugenini kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON . Henock Inonga wa Simba hakupata bahati ya kucheza mchezo huo licha ya kupangwa kwenye kikosi Cha DR Congo cha hapo jana.