NKOMA ABWAGA MANYANGA YANGA PRINCESS
Klabu ya Yanga imethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake, Yanga Pirincess, Sebastian Nkoma kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Uongozi wa Yanga unamshukuru Kocha Mkoma kwa kazi yake kipindi chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya Wanawake.
Kwa sasa benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka mwisho wa msimu huu.