Yanga yazindua tawi DR Congo


Historia Inaandikwa Kwa Wananchi: Klabu ya Yanga inaenda kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufungua matawi ya klabu hiyo Nchini Dr Congo,

Wanachama wapya wa klabu hiyo Nchini DR. Congo wameiomba klabu hiyo ikazindue matawi hayo matatu watakapoenda kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Tp Mazembe,

Kwa mujibu wa katiba mpya ya Yanga, pamoja na vitu vingine tawi litakidhi vigezo kusajiliwa ikiwa limefikisha Wanachama (100),Hivyo basi, matawi yaliyokidhi vigezo ambayo yatazinduliwa yatakuwa 3,

Yanga Sc inakuwa klab ya Kwanza kutoka Afrika Mashariki na kati kuwa na matawi nje ya Nchi yao,Pia inakuwa Miongoni mwa Vilabu Afrika na Duniani vinavyoendeshwa kwa Mfumo wa Wanachama kuwa Matawi nje ya nchi yao,

Klabu ya Yanga itaondoka Nchini Tanzania Leo Alhmisi saa 5 Asubuhi Kuelekea DR. Congo kwa kutumia ndege ya ATCL tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa 2 April 2023,

Team of Citizens Tunasema Soka la Tanzania limekuwa sasa, Limekuwa Bora Mpaka kuwavutia raia wa Nchi Mbalimbali,


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA