Beki la Yanga latoa tamko
Beki wa kati wa Kimataifa wa Yanga Mamadou Doumbia amesema kuwa licha ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza lakini atapambana ili apate nafasi hiyo kama ilivyo kwa mabeki wengine.
Doumbia amesema kuwa "wakati mwingine Soka ni katili sana nimecheza michuano mikubwa na yenye ushindani wa hali ya juu lakini nimekuja huku sichezi.
"Hilo haliwezi kuondoa malengo yangu,najua kwenye soka changamoto ni kawaida na inahitaji moyo wa ujasiri na kutokukata tamaa kwani kila jambo linawakati wake.
"Ninachojua mimi ni beki mzuri ukifika wakati wangu nitacheza na watu wataniona," alisema beki huyo