KILICHOMWONDOA NKOMA YANGA PRINCESS HIKI HAPA

Na Mwandishi Wetu

INASEMEKANA uongozi wa klabu ya Yanga SC umeamua kumfuta kazi kocha wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma ni kutokana na tabia yake ya kutoka kimapenzi na baadhi ya wachezaji wake.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana zinasema kwamba tabia ya kocha huyo ya kuwataka kimapenzi wachezaji wake imechangia kushindwa kuwanoa vema na kupelekea kushika nafasi ya nne kwenye ligi ya wanawake Serengeti Lite.

Uongozi wa Yanga, jana uliamua kumfuta kazi kocha huyo aliyejiunga na Yanga Princess msimu uliopita akichukua nafasi ya Edna Lema, sasa Fred Mbuna atainoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu akisaidiwa na Esther Chabruma "Lunyamila"


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA