Diarra na Aucho kuikosa TP Mazembe
Klabu ya Yanga SC imethibitisha itawakosa kiungo, Khalid Aucho na kipa Djigui Diarra katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi D dhidi ya TP Mazembe Katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Aucho na Diarra watakosekana katika mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizopata katika michezo iliyopita.