Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2025

Clatous Chama kurudi Simba SC

Huenda Clatous Chota Chama akajiunga na Simba SC kwa mara ya tatu tofauti endapo ombi la klabu ya Simba SC litakubaliwa na Singida Black Stars. Simba SC wanahitaji huduma yake, huwenda akajiunga na Simba Sc dirisha dogo la usajili.. Chama alijiunga na Simba SC kwa mara ya kwanza msimu wa 2018 kama mchezaji huru. Akaondoka na kujiunga na RS Berkane ya Morocco lakini mambo hayakua mazuri akarudi Simba SC.. Msimu jana alijiunga na Yanga SC na baadae akatimkia Singida Black Stars. Kama akirudi tena Simba SC basi itakua mara yake ya tatu

Kinachomuweka benchi Kagoma hiki hapa

Yusuf Kagoma hajapata dakika nyingi kwenye AFCON sio kwa sababu hajui bali Miguel Gamondi anavyotaka timu yake icheze ni tofauti na style ya Kagoma. Alphonce Mabula Msanga he was rapid alikuwa kila sehemu ya uwanja, Kagoma ametulia wanaweza kucheza wote pamoja lakini Miroshi anafanya vizuri vizuri kwa hiyo sio lack of quality kwa Kagoma but style of playing ya kocha.

Simba sasa kumchukua beki wa kati wa Singida Black Stars

Simba Sports Club wameanza rasmi mazungumzo ya kina na aliyekuwa nyota wa Singida Black Stars, Antony Tra Bi Tra kwa lengo la kumsajili kama Mchezaji Huru (Free Agent) kuelekea dirisha dogo la usajili. Antony Tra Bi Tra ni miongoni mwa viungo bora waliowahi kuichezea Singida Black Stars na amekuwa akifuatiliwa na Simba SC kwa muda mrefu, hata kabla ya kuwasili Singida. Kuvunjwa kwa mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote kunawapa Simba nafasi ya dhahabu kunasa saini yake bila gharama ya uhamisho. Chanzo cha karibu na klabu kinadai Simba wanahitaji haraka kiungo mwenye uzoefu wa kimataifa kuongeza ushindani wa kikosi kuelekea mechi nzito za ligi na michuano ya kimataifa. Hatua za mwisho za makubaliano zinatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa.

Gamondi awalilia waliopoteza maisha Oktoba 29

Baada ya Tanzania kutinga hatua ya 16 bora AFCON inayoendelea nchini Morocco, kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars, Miguel Gamondi amesema kwamba ushindi walioupata Stars ni maalum kwa watu waliopatwa na majanga ya 29 Oktoba wakati wa uchaguzi. "Hili Heshima kwa yalio ikuta Tanzania Tarehe 29, natoa hesima zangu za Dhati kwa wale wote walio poteza Maisha Yao " Kocha Miguel Gamondi Via BBC

Pedro Goncalves anaumiza kichwa kwa Mwamnyeto

Sasa itakuaje kwa skipper Bakari Mwamnyeto hii performance ya AFCON halafu pale Yanga sio chaguo namba moja. Bila shaka Pedro Goncalves ana furahia kuwa na matatizo ya hivi, Kama Bakari anacheza kwa nidhamu kubwa dhidi ya mataifa makubwa itakuwa vipi akae benchi kwenye mechi kubwa za kimataifa za Yanga. Bacca, Bakari, Mohamed Hussein, Diarra, Dube na Job, sidhani kama kuna ubishi kuhusu kile ambacho wamefanya kwenye haya mashindano na kwanini Yanga wanaendelea kuwa watawala.

Kibabage abadilishana jezi na staa wa Tunisia

Beki wa Taifa Stars, Nickson Kibabage baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Tunisia, alibadilishana jezi na staa wa Tunisia, Ali Maalouli. . Baada ya kubadilishana Kibabage alikiri kuwa Beki huyo amekuwa akimhusudu sana Maalouli na ni shabiki yake mkubwa.

Alphonce Mabula ni yule yule moto wake mwanzo mpaka mwisho

Kwenye hii AFCON ya 2025 Alphonce Mabula amekuja kutulazimisha wote tuwe mashabiki wake na kwenye hilo amefanikiwa, energy aliyoanza nayo mechi ya kwanza ndio hiyo hiyo amemaliza nayo mechi ya mwisho ya makundi. Kati kati ya msitu wq viungo wenye majina makubwa [timu pinzani ] ametoka na rate za [ 6.9 , 6.6 na 7.2 ] kwa kifupi ,hakuna mechi aliyomtukanisha Gamondi na hakuna kiungo wa timu pinzani ametoka uwanjani na filter. Dakika 270 za Alphonce Mabula kwenye AFCON ni darasa la kujitoa hadi nukta ya mwisho kulinda heshima kwa waliokuamini ili kesho uaminiwe tena

Rais Samia aipongeza Taifa Stars

Ninaipongeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu. Heshima hii kubwa kwetu ni matokeo ya maandalizi mazuri na kujituma kwenu katika kila mchezo. Mmeandika historia kubwa kwa Taifa letu na mmeleta furaha kwa Watanzania wote. Hongereni sana. Ninawatakia kila la kheri katika michezo inayofuata.

Uganda nyanya kwa Nigeria AFFON

TIMU ya Uganda imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Nigeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku huu Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco. Mabao ya Super Eagles yamefungwa na mshambuliaji wa Trabzonspor ya Uturuki, Ebere Paul Onuachu dakika ya 28 na kiungo wa Club Brugge ya Ubelgiji, Raphael Onyedika Nwadike mawili dakika ya 62 na 67, wakati bao pekee la The Cranes limefungwa na mshambuliaji wa Vardar ya Macedonia, Rogers Mato Kassim dakika ya 75. Kwa matokeo hayo, Nigeria inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Tunisia yenye pointi nne na zote zinafuzu moja kwa moja Hatua ya 16 Bora. Tanzania iliyomaliza nafasi ya tatu na pointi zake mbili inafuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bora, huku Uganda iliyoshika mkia Kundi C na pointi yake moja safari yake inaishia hapa.

Bao la Feitoto laipeleka Taifa Stars 16 bora AFCON

TANZANIA imeweka rekodi ya kufuzu Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa mara ya kwanza kihistoria licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na Tunisia katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku huu Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco. Tunisia walitangulia kwa bao la dakika ya 43 la mkwaju wa penalti la kiungo Ismaël Seifallah Gharbi wa Braga ya Ureno anayecheza kwa mkopo FC Augsburg ya Ujerumani. Lakini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ akaisawazishia Taifa Stars dakika ya 48 na kuivusha Tanzania Hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza ndani ya Fainali nne, zikiwemo za 1980, 2019 na 2023. Kwa matokeo hayo, Tunisia imemaliza nafasi ya pili na pointi zake nne, nyuma ya vinara, Nigeria wenye pointi tisa hivyo timu zimefuzu moja kwa moja na Tanzania iliyomaliza na pointi mbili inafuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bora. Uganda iliyoshika mkia Kundi C na pointi yake moja safari yake inaishia hapa na wanarejea Kampala kujipanga kwa majukumu m...

Stellenbosch yapata mrithi wa Steve Barker

Stellenbosch wamemchukua legend wa mpira wa Afrika Kusini Gavin Hunt kuchukua nafasi ya Steve Barker ambaye amejiunga na Simba. Gavin alikuwa na nyakati nzuri akiwa kocha wa Supersport ila miaka ya hivi karibuni amekuwa na changamoto ya kupata matokeo mazuri yenye muendelezo, Stellenbosch wanategemea uzoefu wake utawasaidia.

Simon Happygody Msuva; Mfungaji bora wa muda wote Taifa Stars

Bao lake dhidi ya Uganda kwenye AFCON 2025 ni la 21 akiwa na Taifa Stars, na kumfanya @smsuva27 kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Msuva ambaye ni zao la akademi ya @azamfcofficial, anampita Mbwana Samatta mwenye mabao 20. Hapa nazungumzia mabao ya Taifa Stars tu. Mrisho Ngassa anatajwa kama mfungaji bora wa muda wote, lakini sio sahihi. Kwa Taifa Stars, Ngassa ana mabao kumi tu, ambayo hayamfanyi hata kuwemo kwenye tano bora. Katika kuhesabu haya mabao kuna kosa kubwa sana hufanyika. Watu huchanganya mabao ya Taifa Stars na ya Kilimanjaro Stars. Taifa Stars ndio timu ya taifa ya Tanzania, ikijumuisha wachezaji kutoka bara na visiwani. Hii ndio timu inayoshiriki AFCON, Kombe la Dunia na mechi rasmi za kimataifa. Kwenye timu hii, Msuva amefunga mabao 21, na ndio anaongoza. Samatta ana mabao 20, anafuata. Ngassa ana manao 10. Halafu Kilimanjaro Stars ni timu ya Bara, ambayo hushiriki CECAFA Senior Challenge Cup pekee. Kwenye timu hii, Ngassa ana ma...

Phiri kocha mpya wa makipa Simba SC

KLABU ya Simba imemtambulisha Mzambia, Davies Phiri (49) kuwa Kocha wake mpya wa makipa katika benchi jipya la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Steven Robert “Steve” Barker raia wa Afrika Kusini. Taarifa ya Simba katika kurasa zake imetambulisha na kumkaribisha Phiri, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ambaye anajiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea AmaZulu F.C. ya Afrika Kusini. “Karibu Simba SC, Kocha wa Makipa Davies Phiri,” imesema taarifa kwenye kurasa za Simba SC. Phiri kabla ya kuwa kocha amecheza sika ha kulipwa Afrika Kusini akidakia klabu za Durban Stars, Golden Arrows na Kabwe Warriors. Phiri alikuwepo kwenye kikosi cha Zambia kilichofika Nusu Fainali ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 1996 na kufungwa na Tunisia 4–2. Alikuwepo pia kwenye kikosi cha Chipolopolo kilichoshiriki AFCON ya 1998 na kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi D Kiki am ULI’s pointi nne tu na mwaka 2000 pia walipomaliza nafasi ya tatu Kundi C na mwaka 2002 waliposhika mkia, nafasi ya...

Yanga yaanza na Mwanengo

KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji chipukizi, Emmanuel Samuel Mwanengo (22) kuwa mchezaji wake mpya akijiunga na timu hiyo kutoka TRA United ya Tabora. Mwanengo aliibukia Nyangobo FC ya Zanzibar kabla ya kwenda Tajikistan mwaka 2023 ambako alichezea Ravshan Kulob na Vakhsh mwaka 2024, kabla ya kurejea nchini mwaka huu kujiunga na TRA United, zamani Tabora United. Na baada ya kuonyesha uwezo wake katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ndani ya Nusu msimu anahamia kwa Wananchi kuendeleza kampeni ya kushinda mataji.

Simba yamrudisha Ali Salim

Wakati Simba wapo sokoni kutafuta Kipa wa kuziba pengo la Mousa Camara na Yakubu Seleman ambao wote watakosekana kwa muda kidogo. Simba walifikilia kuongeza kipa ambae ni Malimi wa Mtibwa Sugar au Yona Amos wa Pamba jiji. Lakini taarifa mpya ni kwamba Simba wameamua kumchukua Ally Salim Khatolo kipa wao wa zamani ambae anakipiga Dodoma Jiji kutokana na Experience,Ubora na Kuelewa mazingira ya klabu pia alishawahi kucheza dhidi ya mechi kumbe za CAF kama robo fainali dhidi ya Wydad Athletic 

Gamondi alikuwa anapangiwa kikosi pale Yanga- Edo Kumwembe

Mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema kwamba kocha wa sasa wa timu ya taifa, Taifa Stars, Miguel Gamondi wakati anaifundisha Yanga alikuwa anapangiwa kikosi. "Tumuheshimu Bakari Mwamnyeto. Watu wengi huwa wanamdharau nahodha Nondo. Kuanzia katika klabu yake hadi timu ya taifa. Sijui kwanini. Hata hivyo, safari hii amepata muda wa kutukumbusha ubora wake akiwa katika jukwaa kubwa. Nondo anaonyesha uzoefu. Anaonyesha uongozi wake" "Katika mechi zote mbili amekuwa bora. Chini ya Mzungu Gamondi Nondo anafaidika kupangwa pale katikati kwa sababu ya kimo chake. Anacheza kando ya Bacca. Kumbe Gamondi alikuwa na kitu moyoni wakati anaifundisha Yanga SC. Inawezekana alikuwa na shinikizo la kuwapanga zaidi Job na Bacca. Kwanini katika kikosi cha Stars ameamua kwenda na Nondo na Bacca? EDO KUMWEMBE, Mchambuzi WASAFI FM.

Simba ikianza mazoezi na GYM

KIKOSI cha Simba leo kimerejea mazoezini wachezaji wakianza na mazoezi ya gym kujiandaa na michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyoanza jana visiwani Zanzibar.

Tunisia yaifumua Uganda AFCON

TUNISIA imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco. Mabao ya Eagles of Carthage yamefungwa na viungo, Ellyes Joris Skhiri wa Eintracht Frankfurt ya Ujerumani dakika ya 10 na Mohamed Elias Achouri wa FC Copenhagen ya Denmark mawili dakika ya 40 na 64, wakati la The Cranes lilifungwa na mshambuliaji wa APR ya Rwanda, Denis Omedi dakika ya 90’+2. Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi C jana Nigeria iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco. Mabao ya Super Eagles yalifungwa na beki wa Hull City ya England, Oluwasemilogo Adesewo Ibidapo “Semi” Ajayi dakika ya 36 na winga wa Atalanta ya Italia, Ademola Lookman Olajade Alade Ayoola Lookman dakika ya 52, wakati la Taifa Stars limefungwa na kiungo wa Floriana ya Malta, Kokola Charles William M’Mombwa dakika ya 50.

Boli la Stars limewatesa Nigeria mwanzo mwisho AFCON

Anaandika  Ephrahim Mabena Dakika 30 za kipindi cha kwanza zilikuwa tamu sana Kuitazama Stars iliyojaa energy,Kasi na confidence ya juu sana ,Walizua vyema mno na walijaribu kukaa na mipira Kwa dakika kadhaa Nigeria walipata Wakati Mgumu mno kuwafunga stars iliyokuwa na ujasiri mkubwa dakika zile 30 za mwanzo Zuberi Foba ni Golikipa mzuri na ameonyesha MWANGA mzuri kwenye timu ya Taifa licha ya kufungwa lakini amepunguza Idadi ya magoli Height yake ilifanya saves nzuri mbele ya vichwa vya Osimhen na Ajay ambao Kwa kimo na warefu haswa. Ibrahim Bacca Leo ameonyesha namna gani yeye ni sajenti kwenye Taifa,Victor Osimhen amekuwa na Wakati mwingi Mgumu mbele ya Bacca mpaka Kuna Wakati alikuwa Anataka huruma ya mwamuzi, Kiufupi Bacca Leo amekuwa Bora mno akiambatana na Bakari Mwamnyeto wamekuwa na utulivu sana eneo la ulinzi. Victor Osimhen analala akiota jina la Sajenti Ibrahim Bacca,Kila alipotupa miguu na Bacca alikuwa nyuma yake , kiufupi Osimhen kawekwa mifukoni mwa sajenti Bacca Leo N...

Nigeria kwa mbinde yailaza Tanzania 2-1, AFCON

Timu ya taifa ya Nigeria imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwa mbinde dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mchezo wa kundi C kombe la mataifa Afrika, AFCON. Mabao ya Nigeria yamefungwa na Semi Ajayi dakika ya 35 na Ademola Lookman dakika ya 52 wakati goli pekee la Tanzania limefungwa na Charles M'Mombwa dakika ya 50. Kwa kifupi katika mchezo wa leo Taifa Stars inayonolewa na kocha Miguel Gamondi imecheza vizuri na kufufua matumaini ya kutinga hatua inayofuata, ikiwa itasaliwa na mechi mbili dhidi ya Uganda na Tunisia

Bilioni moja kumtoa Allan Okello, Vipers

Wakati Simba na Yanga zinapiga kelele mitandaoni juu ya usajili wa nyota wa kimataifa Allan Okello tayari Vipers wameweka sokoni dau la nyota huyo kwa yeyote atakaye muhitaji Klabu ya hiyo kutoka Uganda inadaiwa kudai zaidi ya Dola 500,000 (≈ Shilingi za Tanzania bilioni 1.3), kiasi kinachojumuisha bonasi ya usajili. Ingawa dau hilo ni kubwa, lakini sio kikwazo kwa Al Ahly Benghazi, ambao wameripotiwa kuwasilisha mezani ofa ya takribani Dola 400,000 (≈ Shilingi za Tanzania bilioni 1.04).

Senegal yaiduwaza Botswana, AFCON

Nicolas Jackson amefunga magoli mawili na kuisaidia Senegal kuibuka na ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa Kundi D dimba la Ibn Batouta. Mabao ya Senegal yamefungwa na Nicolaus Jackson (mawili) dakika ya 40 na 58 na Ndiaye dakika ya 90. MSIMAMO KUNDI D (baada ya mechi za raundi ya kwanza:) 1. Senegal — pointi 3 2. DR Congo — pointi 3 3. Benin — pointi 0 4. Botswana — pointi 0

Stars yapata pigo, kuwakosa Feitoto, Yakoub

Kuelekea mchezo wa Kundi C wa kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025 kati ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Nigeria utakaopigwa leo Desemba 23, 2025 Taifa Stars imepata pigo baada ya golikipa wake muhimu, Yakoub Suleiman kupata jeraha la goti kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo. Stars ambayo itakabiliana Nigeria majira ya saa 2:30 usiku katika dimba la Fez, Morocco pia itakosa huduma ya kiungo, Feisal Salum 'Feitoto' kwa kuoneshwa kadi mbili za njano kwenye mechi tofauti za kufuzu. MATCH DAY | AFCON 2025 15:30 DR Congo vs Benin AI Barid Stadium 18:00 Senegal vs Botswana Ibn Batouta Stadium 20:30 Nigeria vs Tanzania Complexe sportif de Fès 23:00 Tunisia vs Uganda Stade Olympique de Rabat

Nay Dat ni mtoto wa Prince Hoza ajikita kwenye uigizaji

Mtoto wa kwanza wa Prince Hoza ambaye ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kupitia magazeti ya Simba SC ya Msimbazi na Mwanasoka, pia mchambuzi wa michezo aliyepitia vituo kadhaa vya redio, Saida Fikiri Salum Hoza a k a yake Nay Dat,ameamua kujikita katika sanaa ya maigizo. Akizungumza na mtandao huu ambao pia umilikiwa na baba yake (Prince Hoza) ameweka wazi kwamba yeye kwa sasa ni msanii na tayari yupo kambini Kiluvya na kikundi chao akitayarisha kazi ambazo zitawarudisha mjini wakiwa na mafanikio kibao. Saida ambaye ni mtoto wa kwanza wa Hoza akiwa amezaliwa peke yake kwa mama yake Rosemary Daudi (marehemu) lakini akiwa na wadogo zake watatu na jumla kuwa wanne kwa baba yao, amedai kwamba sanaa ameirithi toka kwa baba yake kwani kabla hajawa mwandishi, alianza kwenye uigizaji. Hoza alikuwa kwenye kikundi cha Nyati Cultural Troupe cha Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam akiwa kama mwalimu, hivyo anaamini kwamba yeye sanaa amezaliwa nayo. Mambo Uwanjani Blog itawaletea makala...

Misri yatoka nyuma na kuibuka mbabe mbele ya Zimbabwe, AFCON

TIMU ya Misri imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) usiku wa jana Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco. Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube Mpumelelo alianza kuifungia The Warriors dakika 20, kabla ya The Pharaohs kuzinduka kwa mabao ya washambuliaji wake wanaocheza England, Omar Khaled Mohamed Abdelsalam Marmoush wa Manchester City dakika ya 64 na Mohamed “Mo” Salah Hamed Mahrous Ghaly wa Liverpool dakika ya 90’+1. Ikumbukwe mchezo mwingine wa kwanza wa Kundi B jana Afrika Kusini ilishindi 2-1 dhidi ya jirani zao, Angola Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech. Mabao ya Bafana Bafana yalifungwa na winga wa Orlando Pirates, Oswin Reagan Appollis dakika ya 21 na mshambuliaji wa Burnley ya England, Lyle Brent Foster dakika ya 79, wakati la Palancas Negras limefungwa na Manuel Luís da Silva Cafumana anayecheza kwa mkopo Kocaelispor ya Uturuki kutoka Maccabi Haifa ya Israel dakika ya 35.

Afrika Kusini yaichakaza Angola

TIMU ya Afrika Kusini imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jirani zao, Angola katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco. Mabao ya Bafana Bafana yamefungwa na winga wa Orlando Pirates, Oswin Reagan Appollis dakika ya 21 na mshambuliaji wa Burnley ya England, Lyle Brent Foster dakika ya 79, wakati la Palancas Negras limefungwa na Manuel Luís da Silva Cafumana anayecheza kwa mkopo Kocaelispor ya Uturuki kutoka Maccabi Haifa ya Israel dakika ya 35. Mchezo mwingine wa Kundi B unafuatia usiku huu kati ya Misri na Zimbabwe Uwanja wa Adrar mjini Agadir.