Anaandika Ephrahim Mabena
Dakika 30 za kipindi cha kwanza zilikuwa tamu sana Kuitazama Stars iliyojaa energy,Kasi na confidence ya juu sana ,Walizua vyema mno na walijaribu kukaa na mipira Kwa dakika kadhaa
Nigeria walipata Wakati Mgumu mno kuwafunga stars iliyokuwa na ujasiri mkubwa dakika zile 30 za mwanzo
Zuberi Foba ni Golikipa mzuri na ameonyesha MWANGA mzuri kwenye timu ya Taifa licha ya kufungwa lakini amepunguza Idadi ya magoli Height yake ilifanya saves nzuri mbele ya vichwa vya Osimhen na Ajay ambao Kwa kimo na warefu haswa.
Ibrahim Bacca Leo ameonyesha namna gani yeye ni sajenti kwenye Taifa,Victor Osimhen amekuwa na Wakati mwingi Mgumu mbele ya Bacca mpaka Kuna Wakati alikuwa Anataka huruma ya mwamuzi, Kiufupi Bacca Leo amekuwa Bora mno akiambatana na Bakari Mwamnyeto wamekuwa na utulivu sana eneo la ulinzi.
Victor Osimhen analala akiota jina la Sajenti Ibrahim Bacca,Kila alipotupa miguu na Bacca alikuwa nyuma yake , kiufupi Osimhen kawekwa mifukoni mwa sajenti Bacca Leo
Novatus Dismas Leo pasi nyingi alikuwa anapoteza kwenye eneo la kiungo
Ule mguu wa Kushoto wa Chukweze umejaa Sanaa kubwa sana ya kutembea na mpira, walinzi wa Stars waliteseka sana juu yake.
Nigeria wameshinda lakini furaha haipo ,Stars wamewapa mechi ngumu sana mastaa wa Nigeria
Kelvin John upewe nini pale kufunga tena dakika za jioooni zile
Mkeka wa mwanetu Davido wa Both team to score umetiki
Anyways tumefungwa ila furaha ya Vijana wetu kuwaona wakivuja jasho Bila uoga Wala papara


