Mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema kwamba kocha wa sasa wa timu ya taifa, Taifa Stars, Miguel Gamondi wakati anaifundisha Yanga alikuwa anapangiwa kikosi.
"Tumuheshimu Bakari Mwamnyeto. Watu wengi huwa wanamdharau nahodha Nondo. Kuanzia katika klabu yake hadi timu ya taifa. Sijui kwanini. Hata hivyo, safari hii amepata muda wa kutukumbusha ubora wake akiwa katika jukwaa kubwa. Nondo anaonyesha uzoefu. Anaonyesha uongozi wake"
"Katika mechi zote mbili amekuwa bora. Chini ya Mzungu Gamondi Nondo anafaidika kupangwa pale katikati kwa sababu ya kimo chake. Anacheza kando ya Bacca. Kumbe Gamondi alikuwa na kitu moyoni wakati anaifundisha Yanga SC. Inawezekana alikuwa na shinikizo la kuwapanga zaidi Job na Bacca. Kwanini katika kikosi cha Stars ameamua kwenda na Nondo na Bacca?
EDO KUMWEMBE, Mchambuzi WASAFI FM.
