Mtoto wa kwanza wa Prince Hoza ambaye ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kupitia magazeti ya Simba SC ya Msimbazi na Mwanasoka, pia mchambuzi wa michezo aliyepitia vituo kadhaa vya redio, Saida Fikiri Salum Hoza a k a yake Nay Dat,ameamua kujikita katika sanaa ya maigizo.
Akizungumza na mtandao huu ambao pia umilikiwa na baba yake (Prince Hoza) ameweka wazi kwamba yeye kwa sasa ni msanii na tayari yupo kambini Kiluvya na kikundi chao akitayarisha kazi ambazo zitawarudisha mjini wakiwa na mafanikio kibao.
Saida ambaye ni mtoto wa kwanza wa Hoza akiwa amezaliwa peke yake kwa mama yake Rosemary Daudi (marehemu) lakini akiwa na wadogo zake watatu na jumla kuwa wanne kwa baba yao, amedai kwamba sanaa ameirithi toka kwa baba yake kwani kabla hajawa mwandishi, alianza kwenye uigizaji.
Hoza alikuwa kwenye kikundi cha Nyati Cultural Troupe cha Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam akiwa kama mwalimu, hivyo anaamini kwamba yeye sanaa amezaliwa nayo.
Mambo Uwanjani Blog itawaletea makala maalum ikimuhusu Saida Fikiri Salum Hoza.







