Timu ya taifa ya Nigeria imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwa mbinde dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mchezo wa kundi C kombe la mataifa Afrika, AFCON.
Mabao ya Nigeria yamefungwa na Semi Ajayi dakika ya 35 na Ademola Lookman dakika ya 52 wakati goli pekee la Tanzania limefungwa na Charles M'Mombwa dakika ya 50.
Kwa kifupi katika mchezo wa leo Taifa Stars inayonolewa na kocha Miguel Gamondi imecheza vizuri na kufufua matumaini ya kutinga hatua inayofuata, ikiwa itasaliwa na mechi mbili dhidi ya Uganda na Tunisia
