Wakati Simba na Yanga zinapiga kelele mitandaoni juu ya usajili wa nyota wa kimataifa Allan Okello tayari Vipers wameweka sokoni dau la nyota huyo kwa yeyote atakaye muhitaji
Klabu ya hiyo kutoka Uganda inadaiwa kudai zaidi ya Dola 500,000 (≈ Shilingi za Tanzania bilioni 1.3), kiasi kinachojumuisha bonasi ya usajili.
Ingawa dau hilo ni kubwa, lakini sio kikwazo kwa Al Ahly Benghazi, ambao wameripotiwa kuwasilisha mezani ofa ya takribani Dola 400,000 (≈ Shilingi za Tanzania bilioni 1.04).
