Kuelekea mchezo wa Kundi C wa kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025 kati ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Nigeria utakaopigwa leo Desemba 23, 2025 Taifa Stars imepata pigo baada ya golikipa wake muhimu, Yakoub Suleiman kupata jeraha la goti kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo.
Stars ambayo itakabiliana Nigeria majira ya saa 2:30 usiku katika dimba la Fez, Morocco pia itakosa huduma ya kiungo, Feisal Salum 'Feitoto' kwa kuoneshwa kadi mbili za njano kwenye mechi tofauti za kufuzu.
MATCH DAY | AFCON 2025
15:30 DR Congo vs Benin
AI Barid Stadium
18:00 Senegal vs Botswana
Ibn Batouta Stadium
20:30 Nigeria vs Tanzania
Complexe sportif de Fès
23:00 Tunisia vs Uganda
Stade Olympique de Rabat
